Saturday, June 30, 2012

Taswira Mbalimbali Za Jinsi Hali Ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Steven Ulimboka inavyoimarika

 

 


 
  Hali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili (MNH), Kitengo cha mMifupa (MOI) aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru Kama aonekanavyo pichani juu.Picha na Mdau Dande Francis

 

TASWIRA KUTOKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) MARA BAADA YA WANAFUNZI WA MWAKA WA 3 KUMALIZA MASOMO YAO LEO

 Wanafunzi wa Mwaka wa tatu wa fani mbalimbali wakiwa katika foleni ya kurudisha vitambulisho vya chuo mara baada ya Kumaliza miaka 3 ya masomo yao ya shahada ya kwanza
 Mwanafunzi wa UDOM akiwa tayari kurudi nyumbani kwao mara baada ya kumaliza mitihani yake
 Kama kawaida Ifikapo kipindi hiki cha kumaliza muhula usafiri unasumbua na teksi ndio muda wao na hapa zikiwa zimehamia chuoni kabisa na kusubiri wateja
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakisubiri daladala ili kuelekea mjini jioni ya leo.Katika Kipindi hiki Cha Wanafunzi kumaliza muhula na kufunga chuo na wengine kumaliza kabisa usafiri huwa ni wa taabu sana na ndio msemo wa kufa kufaana unapotimia mara baada ya teksi kuchukua nafasi katika kipindi hiki cha kufunga chuo
 
 
 

Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara Anusurika Kifo Katika Ajali

 
 Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara,
---
 Waziri wa Habari Utamaduni Vijana na Michezo Dkt. Finella Mukangara,amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea leo Igunga mkoani Tabora wakati akiwa safarini kuelekea Mwanza akitokea Dodoma.

Gari la Waziri Dk. Mukangara linadaiwa kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulipita roli la mizigo na kutaka kugongana uso kwa uso na basi la Green Sta lililokuwa likitokea Mwanza.

Waziri, Msaidizi wake na dereva walipata majeraha na kutibiwa katika Hospitali ya Nzega Mkoani Tabora
 

MABONDIA WAAHIDIWA BAISKELI

mabondia wa bigright boxing wakiwa mazoezini
kocha wa bigright boxing ibrahim akiwanoa vijana
Mabondia wa klabu ya mazoezi ya bigright ya mwananyamala wameahidiwa baiskel na katibu kata wa vijana wa CCM kinondoni REHEMA MBEGU ili ziwasaidie kwenda mashuleni mwao na mazoezini,Rehema mbegu mara nyingi huwa yupo karibu sana na vijana hao katika ushauri na kuwasaidia chakula na vinywaji wakati wakijiandaa na mashindano mbalimbali ,safari hii ameamua kutoa baiskeli ili kuhamasisha ushindani zaidi na kuwapa moyo vijana kupenda zaidi michezo kuliko vijiwe.

Baada ya kuhakikishiwa kuwa kila bondia atakae shinda toka klabu ya ngumi ya bigright atazawadiwa baskeli,wameahidi kukatika mikono ulingoni yaani ni lazima washinde na wamebadilisha mfumo mzima wa mazoezi,kwa sasa wapo pamoja,kikambi zaidi nyumbani kwa kocha wao Ibrahim bigright na kuongeza muda zaidi wa mazoezi kwa sasa wanafanya mara tatu hadi nne kwa siku.

Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni july 15 DDC-kariakoo ni Issa Omar(bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele toka kambi ya matumla katika uzani wa fly,Mwaite juma toka bigright boxing atapigana na mkongwe Anthony Mathias katika uzani wa bantam.

Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa kati ya JUMA FUNDI wa keko na BAINA MAZOLA wa mabibo toka kambi ya mzazi
 
mapambano hayo yameandaliwa na kaike siraju na kusimamiwa na TPBO
 

RAIS AOMBOLEZA KIFO CHA MAMA MZAZI WA WAZIRI STEPHEN WASIRA LEO

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira jijini Dar es salaam leo, baada ya heshima za mwisho mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea wilayani Bunda kwa maziko.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Gaudencia Kabaka, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, na wanafamilia wa wafiwa  wakitoa heshima za mwisho kwa mama wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Stephen Wassira (kushoto kwa Rais) , Marehemu Esther Mgaya Mankaba, leo nyumbani kwa Mhe Wassira     jijini  Dar es salaam leo.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment