Pages

Monday, May 28, 2012

 

 

 

 

EURO 2012 COUNTDOWN: VIJUE VIWANJA, RATIBA NA MAKUNDI YA MICHUANO YA UBINGWA WA MATAIFA YA ULAYA


KIEV - Olympic Stadium, 60,000

Huu ndio uwanja wa taifa wa Ukraine. Ndio uwanja utakaotumika sana kwenye michuano hii. Kwa sasa umeshamalizia matengenezo makubwa kwa ajili ya matayarisho ya mechi za makundi, robo fainali na fainali yenyewe.


Dynamo Kiev ndio wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.


RATIBA YA MECHI ZA MAKUNDI KWENYE DIMBA HILI
Monday, June 11 - Ukraine v Sweden (1945)
Friday, June 15 - Sweden v England (1700)
Tuesday, June 19 - Sweden v France (1945)

ROBO FAINALI
Sunday, June 24 - Winner D v Runner-up C (1945)

FINAL


Sunday, July 1 - Winner SF1 v Winner SF2 (1945).
Kiev: Olympic Stadium
Kiev: Olympic Stadium -Unaingiza watu 60,000
LVIV - New Lviv Stadium - Watu 30,000
Uwanja huu upo katika mji ambao zamani ulikuwa moja ya sehemu ya Poland na ndio eneo lilipozaliwa shirikisho la soka la Poland- na unatumiwa na klabu ya FC Karpaty kama uwanja wa nyumbani.
MECHI ZA MAKUNDI ZITAKAZOCHEZWA HAPA

Saturday, June 9: Germany v Portugal (1945)
Wednesday, June 13: Denmark v Portugal (1700)
Sunday, June 17: Denmark v Germany (1945)


Lviv: New Lviv Stadium
Lviv: New Lviv Stadium


Kharhiv: Metalist Stadium
Kharhiv: Metalist Stadium

KHARKIV - Metalist Stadium, - Watu 30,000
Uwanja huu una historia ya kutengenza watu 40 ambao wote wameshavaa medali za Olympic, upo katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Uwanja ulijengwa mwaka 1962.

MECHI ZA MAKUNDI ZITAKAZOCHEZWA HAPA
Saturday, June 9: Holland v Denmark (1700)
Wednesday, June 13: Holland v Germany (1945)
Sunday, June 17: Portugal v Holland (1945)




DONETSK - Donbass Arena - Watu 50,000
Uwanja wa kisasa kabisa, ulijengwa kwa kutumia £255million na kumalizika mwaka 2009, utachezewa mechi tatu za makundi, robo fainali na nusu fainali.

Huu ni uwanja wa nyumbani wa Shakhtar Donetsk.

MECHI ZA MAKUNDI ZITAKAZOCHEZWA HAPA
Monday, June 11: France v England (1700)
Friday, June 15: Ukraine v France (1945)
Tuesday, June 19: England v Ukraine (1945)


ROBO FAINALI
Saturday, June 23: Winner C v Runner-up D (1945)


NUSU FAINALI
Wednesday, June 27: Winner QF1 v Winner QF3 (1945)



Donetsk: Donbass Arena
Donetsk: Donbass Arena
     

POLAND

WARSAW - Uwanja wa Taifa (Umejengwa kwa ajili ya Euro 2012): 50,000

Michuano ya Euro 2012 itafunguliwa katika uwanja mpya wa taifa wa Poland, uwanja huu umejengwa kwa kutumia £255million zikiwa ni pesa za serikali.

Uwanja huu baada ya Euro unatajiwa kutumiwa na timu za Legia Warsaw na Polonia Warsaw kwa mechi kubwa tu - lakini sio kila mechi.


MECHI ZA MAKUNDI ZITAKAZOCHEZWA HAPA
Friday, June 8 - Poland v Greece (1700)
Tuesday, June 12 - Poland v Russia (1945)
Saturday, June 16: Greece v Russia (1945)
 

QUARTER-FINAL
Thursday, June 21 - Winner A v Runner-up B (1945)
SEMI-FINAL
Thursday, June 28 - Winner QF2 v Winner QF4 (1945)

Warsaw: The National Stadium
Warsaw: The National Stadium






GDANSK - PGE Arena, 40,000

Uwanja wa manispaa - unaotumiwa na klabu ya Lechia Gdansk.

MECHI ZA MAKUNDI KWENYE DIMBA HILI
Sunday, June 10 - Spain v Italy (1700)
Thursday, June 14 - Spain v Republic of Ireland (1945)
Monday, June 18 - Croatia v Spain (1945)
 

ROBO FAINALI
Friday, June 22 - Winner B v Runner-up A (1945)

Gdansk: The PGE Arena
Gdansk: The PGE Arena


POZNAN - City Stadium, 40,000

Uwanja wa nyumbani wa KKS Lech Poznan na Warta Poznan, ulijengwa mwaka 1980 lakini sasa umefanyiwa matengenezo makubwa mbele ya fainali hizi.

MECHI ZA MAKUNDI
Sunday, June 10 - Republic of Ireland v Croatia (1945)
Thursday, June 14 - Italy v Croatia (1700)
Monday, June 18 - Italy v Republic of Ireland (1945)

Poznan: City Stadium
Poznan: City Stadium


WROCLAW - Municipal Stadium, 40,000

MECHI ZA MAKUNDI ZITAZOPIGWA HAPA
Friday, June 8 - Russia v Czech Republic (1945)
Tuesday, June 12 - Greece v Czech Republic (1700)
Saturday, June 16 - Czech Republic v Poland (1945)

Wroclaw: Municipal Stadium

OXLADE-CHAMBERLAIN: UFUPI ULITISHIA MAISHA YANGU YA SOKA - LAKINI XAVI NA INIESTA WALINIONYESHA SAIZI YA KIMO SIO MUHIMU

Wakati Andres Iniesta na Xavi walipokuwa busy wakishinda Euro 2008, Alex Oxlade-Chamberlain alikuwa hana uhakika kwamba ataweza kucheza soka pale Southampton, achana kabisa na kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya England katika michuano ya EURO.

Lakini kuingizwa kwa mchezaji huyu kwenye kikosi cha Roy Hodgson kwa ajili ya Euro 2012, kunamfanya awe na deni kubwa kwa viungo wa Kihispania kwa kile walichokifanya mwaka ule.

Wakati huo, Oxlade-Chamberlain hakuwa hata haonekani kama ataweza kupewa mkataba wa kiuwanafunzi na Southampton kwa sababu alikuwa na umbo dogo sana. Mwaka mmoja baadae, alipofikisha miaka 15, alianza kutafakari nini atafanya huko mbele kama sio mchezaji wa soka.

Lakini miaka minne tangu Euro 2008, Spain wametawala soka la dunia, na wachezaji kama David Silva mwenye kimo cha 5ft 8in, David Villa - 5ft 7in, na Pedro mwenye urefu wa 5ft sawa na roho ya timu hiyo Xavi na Iniesta ambao wote nao wana urefu wa futi 5 - lakini wameiongoza timu yao ya tifa pamoja na klabu yao Barcelona kushinda makombe mawili ya ulaya, makombe mawili ya dunia ya nazi ya vilabu, na makombe matatu ya La Liga.


"Huhitaji kuangalia mbali zaidi ya Xavi na Iniesta," anasema Oxlade Chamberlain ambaye sasa ana miaka 18 na urefu wa 5ft 11in.
"Kama ukiwa na akili ya soka na kuuchezea mpira na touch yako ni nzuri, na ukiwa na maumbo kama yetu huwezi kuruhusu kukumbana au kwenda kwenda vita ya nguvu dimbani.
"Kwa mfano Iniesta aende kwenye kugombea mpira na kiungo mrefu wa kati mwenye manguvu, naamini kwenye raundi nane kati ya 10 atapoteza. Lakini Iniesta ana akili kuliko, anatumia touch yake ya kwanza kumpita mchezaji  pinzani na kukaa mbele, hivyo mpinzani wake itabidi amchezee faulo au amuache aende mbele baada ya kupitwa.
"Inabidi ucheze aina hiyo ya soka kutokana na jinsi ulivyo mwenyewe na nafikiri hilo linakuja naturally. Ukijifunza kila siku, haijalishi una nguvu kiasi gani, inabidi ucheze kwa mtindo aina ya Iniesta.
"Ni mafundisho ya soka kwa yoyote, jaribu tu kuwaangalia Barcelona wanavyocheza. Namuangalia Lionel Messi, Iniesta na hata Cesc Fabregas. Siku zote napata vingi vya kujifunza kutoka wengine."

Mchezaji mwenzie wa Arsenal Aaron Ramsey anaamini kabisa atajifunza zaidi kwenye Euro 2012, akisema: "Alex amekuwa na msimu mzuri. Ni mdogo, anafurahisha kumuangalia, kwa hakika kabisa ana wakati mzuri sana huko mbele na nilifurahi sana alipoitwa.
"Kwa hakika kabisa amekuwa na anaweza kucheza kwenye hatua ya kimataifa."

Oxlade-Chamberlain alianza atleast kupata kimo alipofikisha miaka 16, wakati Southampton walipomuingiza kwenye kikosi cha timu ya watoto. Na hapo ndipo alipoanza kuondoa uoga kidogo kwenye kupambana na wachezaji wenye miili mikubwa.


Na katika kuonyesha kwamba ameanza kufaulu mafunzo aliyokuwa akiyapata kwa kuwaangalia akina Iniesta, aliweza kupambana na kumsumbua sana Mark van Bommel kwenye mechi ya Champions League dhidi ya AC Milan mwezi wa 3 mwaka huu - wakati kinda  huyo alipocheza nafasi ya kiungo wa kati huku akipambana na mholanzi huyo - kwa hakika alionyesha kweli anaweza kupambbana vita yoyote na nguvu.

Siku zote amekuwa akipewa sapoti ya nguvu, na baba yake Mark ambaye aliichezea England kwenye miaka ya 80.

Mark alimwambia mwanae asiwe na wasiwasi kuhusu kutokuwa na na kimo kirefu, na badala yake aweke umakini katika kujifunza kuwa na ufundi na matokeo yake Oxlade Chamberlain ameendelea na kuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa soka.

"Kama wewe ni mchezaji mwenye umbo dogo, inabidi uzoee kucheza na ubongo  wako zaidi na kujifunza mbinu tofauti,: anasema Alex. "Na kama ukiweza kufanya hivyo, basi hilo litakuongezea uwezo zaidi utakapokuwa mkubwa."

Ikiwa Oxlade-Chamberlain atafanikiwa kuichezea England huko Ukraine, sio wazazi wake wala kaka yake, Christian, watakuwa pale kuangalia hilo.

Baba yake alisema wiki iliyopita kwamba uoga wa ubaguzi wa rangi umeizuia familia hiyo kwenda nchini humo.

 Alex na baba yake George  Eastham senior na junior, Brian na Nigel Clough, na Frank Lampard  senior na junior ni muunganiko wa mababa na watoto zao ambao wote kwa pamoja wameiwakilisha timu yao ya taifa.

"Soka siku zote imekuwa sehemu ya maisha yangu, baba yangu alicheza," anasema Chamberlain. "Unapomuona baba yako anacheza na wewe utamani ujaribu na mie nilijaribu na nikapenda. Baba yangu hakuwahi kunilazimisha kucheza.
"Nilikuwa nafurahia kucheza na baba yangu alinisaidia. Alitumia muda mwingi kunifundisha, kunipeleka viwanjani na kunionyesha vitu tofauti pamoja na kuniongezea vitu kwenye mchezo wangu kiufundi. Siku zote alinifanya niupende zaidi mchezo huu."

Mark - baba wa Oxlade bado anafanya kazi nzuri katika kumuendeleza mwanae Chamberlain na soka lake kwa kukaa kuangalia michezo iliyopita kwenye DVD.
"Mimi na baba yangu huwa tunakaa pamoja sitting room na kuangalia michezo iliyopita kwenye DVD, tunafurahia sana kuangalia mpira, napenda kuangalia mechi nilizocheza na kujifunza zaidi kwa kuangalia kitu gani nafanya vizuri nikoreshe na wapi nakosea ili nisahihishe. Baba huwa ananiambia vitu tofauti na kunisahihisha ninapokosea. Tunaongea na kusikilizana na mwishoe nazidi kujifunza zaidi." - Alex

EURO 2012 COUNTDOWN: TORRES,MATA NDANI DE GEA N

TAFRIJA YA KUWAPONGEZA UDOM SOCIAL KWA KUWA MABINGWA WA LIGI YA KIKAPU ILIYOPEWA JINA LA DODOMA BASKETBALL DEVELOPMENT LEAGUE 2012

Hili ndio Kombe walilokabidhiwa Wachezaji wa Timu ya Mpira wa Kikapu ya UDOM SOCIAL mara baada ya Kuibuka washindi wa kuifunga Timu ya Mipango Katika Fainali ya Ligi ya MPira wa Kikapu Mkoani Dodoma jana
Baadhi ya Wachezaji na Mashabiki wakiwa katika Meza kubwa kwaajili ya kupata chakula cha jioni kwa pamoja ikiwa kama ishara ya upendo na ushirikiano mara baada ya kuibuka washindi.
 Mmoja wa wachezaji akikabidhiwa Dollar 20 za marekani kama zawadi kwa kusaidia timu yake kuweza kuchukua Ubingwa wa ligi hiyo iliyomalizika jana Na UDOM SOCIAL kuibuka washindi 
 Baadhi ya wanafunzi na wapenda michezo wakiwa katika tafrija fupi ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Mpira wa Kikapu Ya UDOM SOCIAL
 Baadhi ya Wachezaji wakiwa katika Picha Na Kombe lao hapo jana katika tafrija fupi ya kuwapongeza kwa kuleta ushindi UDOM
 Kapteni Wa Timu ya UDOM SOCIAL Fred akiwa katika Picha ya pamoja na mchezaji mwenzake Pascal Nsana na kombe katika tafrija fupi ya kuwapongeza iliyofanyika katika cafteria ya breakpoint hapo jana
 Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza (Wa Pili Kushoto) akiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wachezaji na mashabiki wa mpira wa kikapu katika tafriaj fupi ya kuwapongeza wachezaji wa UDOM SOCIAL kuibuka washindi katika ligi hiyo
Baadhi ya Wadau wakiwa katika Meza kuu tayari kwa kusubiria msosi huku wakiendelea kupata vinywaji katika tafrija fupi ya Kuwapongeza wachezaji hao kwa kushinda katika ligi ya mpira wa kikapu iliyomalizika jana na hatimaye UDOM SOCIAL kuibuka Mabingwa.

KAMPENI ZA UCHAGUZI WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI UDOM WAKOSA MVUTO,WANAFUNZI HAWATAKI SIASA

Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akinadi Sera zake kwa wanafunzi wenzake na kuomba kura kwaajili ya wanafunzi kuweza kumchagua ili awe mbunge kutoka katika Kitivo Cha sayansi ya Jamii.
Mwanafunzi mwingine naye aliweza kuomba kura kwa baadhi ya wanafunzi ambao walihudhuria kampeni zake katika kampeni zinazoendelea tayari kwa uchaguzi wa serikali ya wanafunzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 2 june 2012
Hiyo Ndio kambi moja wapo katika kampeni za kuwania nafasi mbalimbali katika serikali ya wanafunzi wa UDOM wakiwa katika kampeni huku wengine wakisubiri kupiga  kampeni kitu ambacho wanafunzi wengi wamepuuzia na kudharau kampeni.
Wanafunzi Wachache waliojitokeza kusikiliza kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika serikali ya wanafunzi UDOM
Meneja Kampeni akiwapigia Debe wagombea wake huku wanafunzi wengi  wakiwa hawana habari na kampeni na kuendelea na mambo yao kama wanavyoonekana pichani
Kuonyesha kwamba Siasa pamoja na Kampeni zimekosa mvuto wakati wagombea wakinadi sera zao hao huku wao wakitaniana kuhusiana na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi hutakavyokuwa na mwamko mdogo huku wengine wakisema hawatapiga kura kabisa kabisa
Hili ndio kundi la watu waliohudhuria kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali katika serikali ya wanafunzi UDOM.

CASTLE LITE YAJA NA BIA YA KOPO

Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TBL,Edith Mushi afafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa Bia ya Kopo ya Castle Lite jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Castle Lite,Pameka Kikuli.
 
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa kasi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa yenye ujazo wa mililita 375.

 Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji kurudisha chupa kila waitumiapo.

Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini, “ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.
 Meneja wa Bia ya Castle Lite,Pameka Kikuli akionyesha kopo mpya zilizojazwa Bia hiyo ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia wanywaji wake kuondoka nayo,wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika leo kwenye kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Jamii wa TBL,Edith Mushi.

WANAHABARI WAKIWA KAZINI KILA MMOJA AKICHUKUA TASWIRA ILIYO BORA

Baadhi ya Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa makini katika kuchukua taswira zilizo bora wakati wakuu wa wilaya na mikoa (Hawapo Pichani) walipotembelea Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) hapo jana
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment